MUDA unakwenda mbio sana, ukitazama kalenda yako utagundua kua umebaki mwezi mmoja pekee kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2023-24 na siku za kufanya usajili pia nazo zinakatika kwa kasi.
Timu zote 16 zitakaporudi kwenye utaratibu na ratiba ya kukutana viwanjani kila wiki kumwaga jasho kuwania alama tatu na kuzuia kufungwa.
Baadhi ya timu zimeshaanza maandalizi yake, kama Azam FC wao mapema tu wameanza kambi kwa ajili ya msimu mpya.
Simba, Yanga na timu zingine bado wanajivutavuta kwenye kuanza maandalizi ya msimu huo mpya ambao matarajio ya wengi ni kuwa unakwenda kuwa wa moto zaidi.
Sambamba na hilo dirisha la usajili nalo linahesabu siku kuelekea mwisho wa mwezi huu ambao utakuwa ni ukomo wake, kama kawaida Simba, Yanga, Azam FC ndio ambao wapo mstari wa mbele.
Tunaona na kusikia habari zao nyingi za usajili, lakini kwa timu zingine pamekuwa na ukimya fulani, huenda wanapiga shoo za kimya kimya.
Sisi tunawakumbusha tu kwamba, hakuna muda ambao utapatikana tena kwao baada ya dirisha hili, wakikosea hapa mwanzo ni sawa na kukosea msimu mzim.
Tumeona wote sajili nyingi za dirisha dogo zimekuwa na mapungufu mengi, tunazishauri klabu zote kufanya usajili wa maana ili kuepuka kelele za kukosa muunganiko msimu ukianza

