KIUNGO wa Yanga Farid Mussa amesema wazi kuwa hakuna urahisi wa kupata namba kwenye kikosi cha Yanga cha sasa, lakini hatokata tamaa na atazidi kupambana.
Farid Mussa alisema: “Kuna ushindani mkubwa wa namba ila nitapambana.”
Farid alisema hii ni baada ya kiraka huyo kutokuonekana kwa muda mrefu uwanjani. Farid Mussa amesisitiza ushindani wa namba uliopo Yanga ni mkubwa kikosini lakini kukata tamaa ni mwiko kwenye mpira.“Nilikuwa majeruhi, ila nimerudi naendelea na maandalizi kama kawaida, suala la kucheza namwachia Kocha Gamondi, mimi napambana kuhakikisha namshawishi ili aweze kunipa nafasi ya kucheza.
“Sijakata tamaa nitapambana kuhakikisha napata nafasi ya kucheza ili kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameipa mafanikio timu japo sio rahisi lakini inawezekana,” alisema Farid Mussa.Chini ya kocha Miguel Gamondi amecheza dakika 26 tu kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC timu yake ikiibuka na ushindani wa mabao 5-0, hivyo amekosekana kwenye mechi nyingine nane walizocheza Yanga, ikiwemo za kimataifa.