FEISAL AKUBALI KUKIPIGA SIMBA

ZIPO tetesi kuhusu Feisal Salum kuwindwa na klabu ya Simba Baada ya kutumika Kwa Msimu mmoja na nusu akiwa na Azam FC.

Hapana taarifa Rasmi juu ya Simba kupeleka ofa Azam FC Kwa ajili ya kumtaka Feisal, lakini Sasa kazi uenda ikawa nyepesi zaidi kwao Baada ya Feisal mwenyewe kuonesha kuwa hana noma kuvaa Uzi wa Simba.FEISAL“Nipo tayari kucheza Simba na nitacheza kwa moyo mmoja, mpira ni kazi yangu na nitacheza timu yoyote, hilo la thamani ya mkataba hilo lipo kwa uongozi wa timu yangu,” amesema Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘ FEI TOTO’ akijibu tetesi za kutakiwa na Simba.

ALICHOSEMA msemaji wa Azam, Hashim Ibwe kuhusu FEI TOTO kuhusishwa na Simba.

“Hatujawahi kuwa wachoyo na mtu ambaye ana muhitaji mchezaji hapa Azam FC, kwa sababu tumekuwa na wachezaji na kuwaacha na kwenda katika klabu mbalimbali akiwemo Aishi (Manula), Kapombe (Shomari), Erasto (Nyoni), Mudathir (Yahya) na Salum Aboubakar.FEISAL“Hatujatangaza ofa juu ya Feisal bali kama kuna klabu au timu ambayo inamuhitaji kiungo huyo tunawakaribisha waje mezani, timu imefanya thamani ya mkataba wa mchezaji huyo na kuona sawa na kiasi hicho.”

Acha ujumbe