Dili la mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum Abdallah kuelekea klabu ya soka ya Azam bado linaonekana kua kizungumkuti kwa pande zote mbili.
Mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum inasemekana amevunja mkataba na klabu yake ambao ulikua unatamatika mwaka 2024 ambao alisaini mwaka 2020 ndani ya klabu hiyo, Mchezaji huyo alifanikiwa kusaini mkataba wa miaka minne ndani ya klabu hiyo.
Kiungo huyo aliye kwenye ubora mkubwa kwasasa ndani ya Yanga taarifa za kuaminika zinasema amevunja mkataba wake na klabu hiyo kwa kulipa kiwango cha pesa ambacho ni thamani ya mkataba huo, Huku ikielezwa klabu ya Azam wamemuekea mshahara mnono ambao ni mra nne ya ambao alikua analipwa ndani ya Yanga.
Klabu ya Azam Fc wamekua wakimuwinda kiungo huyo ndani ya klabu hiyo tangu mwanzoni mwa mwezi wa 11, Na mpaka wakati huu inaonekana klabu hiyo tayari imefanikiwa kwa asilimia 95 kumalizana na mchezaji huyo kutoka Zanzibar visiwa vya karafuu.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga mapema leo zinaeleza kua klabu hiyo imepinga vikali mchezaji huyo kuvunja mkataba ndani ya timu hiyo, Huku klabu ya Yanga ikirudisha kiasi cha pesa ambacho mchezaji huyo amelipa ili kuvunja mkataba na kudai utaratibu haukufuatwa ni kuweka wazi mchezaji huyo ni mali ya Yanga.
Mpaka wakati huu klabu ya soka ya Azam kama inamuhitaji kiungo Feisal Salum inapaswa ikakae mezani na klabu ya Yanga ili kusikiliza klabu hiyo itahitaji kiasi gani kwa mchezaji huyo, Na sio kwa njia ya kuvunja mkataba kama alivyofanya mchezaji huyo kwani hakufuata taratibu za mkataba zinavyosema.

