Hatimaye Pacome Avunja Ukimya, Kisa Dube, Baleke na Chama

KIUNGO wa Yanga, Pacome Zouzoua amezungumza usajili mpya wa kikosi hicho, huku akitoa msimamo wake, kwa Kuwataja Jean Baleke, Prince Dube na Clatous Chama watakaocheza nao eneo la ushambuliaji la mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Aziz KI kwa sasa yupo Afrika Kusini na kikosi hicho ambacho Jumatano kitashuka tena uwanjani kuvaana na TS Galaxy katika mechi ya pili ya Kombe la Mpumalanga, baada ya juzi kulala 2-1 mbele ya FC Augsburg ya Ujerumani, lakini Pacome yupo kwao Ivory Coast kufuatilia hati ya kusafiria.

Pacome amewajibu wale wanaodhani msimu ujao kwa kikosi hicho kutakuwa na vita ya namba baada ya ujio wa kina Chama na wenzake na badala yake alisema mziki umezidi kuimarika.

Pacome aliyemaliza msimu uliopita na mabao saba alisema hakuna vita yoyote ya namba kama ambavyo wengi wanadhani, lakini sasa kila mchezaji anatakiwa kutumia ubora kuisaidia timu.

Pacome alisema, ujio wa Chama, Dube na Baleke kule mbele utaipa nguvu zaidi timu hiyo ili kuwa na uwiano mzuri zaidi wa kufunga tofauti na msimu uliopita kazi hiyo ilifanywa na viungo washambuliaji zaidi.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

“Timu yetu sasa inaweza kuwa na watu wanaoanza watakaofanya vitu vikubwa na waliobaki nje wakiweka nguvu ili wakiingia kuendeleza walipoanzia wenzao, kifupi mziki umekamilika kwa sasa na tunaamini tutafanya makubwa zaidi ndani na kimataifa,” alisema Pacome aliyetua akitokea Asec Mimosas.

“Kikosi sasa kitakuwa na uhakika wa kucheza kwa nguvu na kubadilisha matokeo wakati wowote, kitu kizuri tangu wachezaji wapya wamekuja na kuongeza mzuka kwani sisi tunaishi kama familia na kupeana mikakati ya ushindi.”

KUHUSU CHAMA

Akizungumzia kuanza wote watatu kwa maana ya yeye (Pacome), Chama na Aziz Ki, nyota huyo alisema hatarajii sana, japo anaamini kuna mechi wanaweza kucheza hivyo, lakini mwishowe, watakaopata shida ni timu pinzani kwa kuwa wachezaji wote hao ni bora wanajua namna ya kuufungua ukuta wa wapinzani.

“Haiwezekani kutoa silaha zote vitani, ingawa bado jukumu linabaki kwa kocha, lakini ninachoamini ni kwamba, hatutacheza kwa pamoja labda itegemee na aina ya mechi ili kuwepo na sabu imara itakayoendeleza moto dakika 90 za mchezo,” alisema Pacome anayetarajiwa kuungana na wenzake wiki hii kambini Sauzi.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe