NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mastaa wake wanne wanatarajia kukosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa, dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini utakaopigwa saa 1 usiku leo kwa Mkapa.

Mastaa Wanne Yanga SC Kuwakosa Wasudan

Nabi aliwataja mastaa hao kuwa na beki wa kuliwa Djuma Shaban, kiungo wa chini Khalid Aucho, Bernard Morrison na Joyce Lomalisa ambao watakosekana kutokana na afya zao kutokuwa sawa.

Leo Jumamosi, Uwanja wa Mkapa Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili wa marudio dhidi ya Zalan FC baada ya ule wa awali kushinda mabao 4-0.

Mastaa Wanne Yanga SC Kuwakosa Wasudan

Nabi amesema:”Kuna wachezaji wanatarajia kuukosa mchezo wetu dhidi ya Zalan mara baada ya kuwapumzisha kutokana na majeraha ambayo walipata.

Aucho, Lomalisa,Moloko na Morrison ambao wote walipata majeraha katika michezo yetu iliyopita hivyo wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Mastaa Wanne Yanga SC Kuwakosa Wasudan

“Kuhusu maandalizi kiujumla tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu na wachezaji waliopo wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo,”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa