FAMILIA ya bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku imemuombea ushindi mkubwa bondia huyo kuelekea katika pambano lake kutetea mkanda wa UBO  dhidi ya Abdo Khaled wa Misr litakalofanyika Septemba 24 mkoani Mtwara.

Familia hiyo ambayo inapatikana katika kijiji cha Kiparang’anda B mkoani Pwani wamemtakia ushindi kwenye pambano hilo lililopewa jina la Ubabe Ubabe 2 linalotarajia kufanyika   kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Babu wa bondia huyo, Iman  Rubaha ambaye ni mwenyekiti wa jiji cha Kiparang’anda B alisema kuwa  wanamtakia ushindi mkubwa bondia katika pambano hilo kutokana na anatokea kwenye asili yao ya akina Rubaha na amekuwa akiwatembelea mara mara kwa mara lakini kama Watanzania wengine wanavyombea ushindi kwenye pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu nchini.

“Hapa Kiparang’anda ndiyo sehemu yenye asili ya Twaha Kasim Rubaha ambaye maarufu kama Kiduku, uhusiano wangu na Kiduku ni mjukuu wangu, sapoti yetu kubwa kwanza ni kumuobea dua ili aweze kushinda pambano lake la Mtwara na mara zote anakuwa na pambano huwa huwa tunafanya hivyo.”

 

“Lakini siyo kwamba huwa tufanya peke yetu lakini watu wa hapa Kiparang’anda kwenye asili yake na wakazi wa Wilaya ya Mkuanga wamekuwa wakimuombea dua kwa kuwa ni kijana wao kama ilivyokuwa kwa Watanzania wengine,” alisema Rubaha.

Kwa upande wa kaka bondia huyo Ahamada Yakubu alisema kuwa mchezo wa ngumu kwa Kiduku ameanza tangu akiwa kijana mdogo kutokana na tabia yake ya kupenda ugomvi kabla ya kuingia kwenye mchezo huo ambapo watamtakia ushindi kutokana na kuamini kwenye uwezo wake akiwa ndani ya ulingo.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa