Potter na Chelsea yake wanajiapanga kuingia  kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa Borrusia Dortmund Jude Bellingham. Jude ambaye ana miaka 19 ni mmoja wa wachezaji wanaotambuliwa sana barani Ulaya ambaye aliivutia Dortmund katika mechi 15 alizocheza.

 

Potter Anamtaka Bellingham

Huku Liverpool na Manchester United wakiwa tayari wametajwa kuwa na nia ya kumsajili kinda huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 100, gazeti la The Sun limeripoti kuwa The Blues hao sasa wapo kwenye mchanganyiko huo wa kumtaka mchezaji huyo.

Mabadiliko makubwa katika uwanja wa Stamford Bridge yamemfanya mmiliki mpya Mmarekani Todd Boehly kutia saini pauni milioni 250 za uhamisho unaokuja, akiimarisha maeneo ya ulinzi na mashambulizi ya kikosi.

Kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel aliondolewa kikosini hapo huku Graham Potter akichukua mikoba yake, Kocha huyo ambaye ni raia wa Kiingereza amekuwa akivutiwa na Jude Bellingham.

 

Potter Anamtaka Bellingham

Kupata mbadala N’golo Kante na Jorginho katika eneo la kiungo kunatarajiwa kuwa kipaumbele kwa meneja huyo wa zamani wa Brighton  msimu ujao wa joto, Ambapo mchezaji huyo wa Borrusia Dortmund ana kandarasi na klabu hiyo hadi 2025 hata hivyo Chelsea watahitaji kuweka ofa kubwa mezani kuwazidi wapinzani wao wa Premier League.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa