NAHODHA Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein amesema kuwa Simba SC ni timu kubwa ya mataji hivyo wataenda kupambana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Nyasa Big Bullet.

Mchezo huo utapigwa kesho jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar huku Simba SC wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyopata kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini.

Nahodha Simba SC aahidi ushindi

Mohamed Hussein alisema kuwa “Kikubwa ni kuendelea kupambana ili tupate matokeo na kuingia kwenye hatua inayofuata, taratibu tutakuwa tunaelekea kwenye malengo yetu.

“Natoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki na tunaahidi kufanya vizuri na kupambana kwa ajili ya viongozi, mashabiki na sisi wenyewe kwani mpira ndio maisha yetu.

Nahodha Simba SC aahidi ushindi

“Kikubwa tunachozungumza tukiwa kambini ni kutengeneza kitu kimoja, utamaduni wa klabu na malengo ya klabu kwa msimu husika, Simba ni timu ya mataji lakini pia timu ya mafanikio.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa