HATIMAYE kocha msaidizi wa Simba SC Seleman Matola ameondoka kwenye klabu hiyo na amethibitisha hilo yeye mwenyewe wakati akiwaaga mashabiki kupitia Simba TV wikiendi iliyopita na kusema kuwa yeye bado ni mali ya Simba.

 

MATOLA

Matola alisema kuwa, umefika wakati wa Kwenda kuongeza ujuzi wa taaluma yake ya ukocha wa Caf Diploma A na masomo hayo yatadumu kwa takribani mwaka mmoja.

Akizungumzia safari yake hiyo Matola alisema, anaondoka kwenye klabu hiyo akiwa bado ni muajiriwa wa Simba na ana mkataba na timu hiyo na hata suala ya kwenda kusoma ni Simba wenyewe wamelipia gharama za kupata kozi hiyo.

Ingawa alishindwa kuweka wazi kama akimaliza masomo hayo atarejea tena kwenye klabu hiyo au itakuwa ndiyo kwaheri kwa kuwa maamuzi ya hilo yapo chini ya viongozi.

 

MATOLA

“Kwanza nishukuru kwa nafasi ambayo nimepewa na viongozi kwenda kusoma hii kozi ambayo kimsingi wao wamelipia kila kitu. Kwahiyo kuanzia kesho (leo) nitaanza masomo yangu.

“Naondoka kwenye timu nikiwa bado ni muajiriwa wa Simba kwa maana nina mkataba na klabu hii. Sasa suala la kurudi au kutorudi hili litakuja baadae huko. Kikubwa wanasimba wajue kuwa mimi bado ni mfanyakazi wa Simba,” alisema

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa