Aliyekua kocha msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Matola amesema kwasasa yupo darasani akisoma na ndio sababu haonekani kwenye benchi la ufundi la klabu ya Simba.
Kocha Matola kwenye benchi la Ufundi la klabu ya Simba kwa kipindi kirefu huku akishirikiana na makocha tofauti tofauti, Lakini kwa kipindi cha karibuni kocha huyo amekua akirudi darasani mara kw amra kwajili ya kuongeza elimu yake.
Kocha huyo amezungumza na kusema kwasasa yupo darasani anasoma huku akisisitiza kua kwasasa hayupo darasani kutafuta leseni tu, Lakini pia anajifunza lugha tofauti tofauti na kocha huyo ametanabaisha lugha anazojifunza ambazo ni Kingereza pamoja na lugha ya Kifaransa.
Kocha Matola amesema aefikia hatua ya kujifunza lugha mbalimbali kutokana na kuhakikisha anaweza kuendaana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, Kwakua kocha huyo ameweka wazi pindi atakapomaliza masomo yake malengo yake yatakua juu sasna hivo ni vizuri kujiandaa mapema.
Baada ya kocha Suleiman Matola kuzungumza maneno hayo wengi wamejiuliza kua kocha huyo ana uwezekano mkubwa huenda asirejee ndani ya klabu ya Simba pindi atakapomaliza masomo yake, Kwani inawezekana kwasasa malengo yake ni kwenda kupata timu kubwa na kua kocha mkuu tofauti na ilivyo ndsni ya Simba kocha huyo akiwa kocha msaidizi.

