Dani Ceballos Kusaini Mkataba Mpya Ndani ya Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Dani Ceballos yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani ulaya.

Kiungo Dani Ceballos amekua akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya klabu ya Real Madrid, Lakini amekua akicheza vizuri kila wakati ambao amekua akipata nafasi ndani ya timu hiyo na klabu hiyo ipo mbioni kumuongezea mkataba mpya mchezaji huyo.ceballosKlabu ya Real Madrid inaelezwa inataka kumpa ofa ya mkataba wa miaka minne kiungo huyo ambaye amekua akionesha ubora ndani ya timu hiyo, Mchezaji huyo ambaye aliwahi kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Arsenal kwasasa amekua moja ya wachezaji vipenzi vya kocha Carlo Ancelotti.

Kiungo Dani Ceballos amekua bora kwenye michezo ya klabu ya Real Madrid siku za karibuni akichukua nafasi ya Tchouameni ambaye alikua majeruhi, Kutokana na ubora ambao ameuonesha kiungo huyo baada ya kuvaa viatu vya Tchouameni imewashawishi klabu ya Real Madrid kutaka kumpatia mkataba mpya.ceballosDani Ceballos ni amekua shujaa asiyeimbwa kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Real Madrid, Lakini amekua kwenye kiwango bora siku za karibuni na kufikia hatua ya kua shujaa anayeimbwa sasa kwani kwenye mchezo wa jana dhidi ya Valencia kiungo huyo aliweza kuimbw ana mashabiki wa klabu ya Real Madrid kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha kwasasa klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.