Mbagala Queens Wababe wa Soka DSM

Timu ya wanawake ya Mbagala Queens imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Kinondoni Queens katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Karume. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Mbagala Queens

Timu hizo mbili zililingana pointi sawa tisa lakini Mbagala Queens ilikuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga 11 na Kinondoni nane na ya kufungwa wote matano na hivyo, Mbagala ikachukua ubingwa kwa tofauti hiyo.

Mbagala iliondoka na zawadi ya kombe. na kitika cha Tsh Laki tano (500,000), mshindi wa pili alipata medali, mpira mmoja na tsh laki tatu (300,000) huku Mshindi wa tatu akijizolea tsh laki mbili (200,000) na. mpira mmoja.  Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi katika fainali hizo jana Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya aliwapongeza mabingwa hao kwa juhudi akisema kuna kitu wameonesha.

 

Kinondoni Queens

Alizitaka timu tatu za juu zilizofanya vizuri kujipanga kuwakilisha vyema katika michuano ya mabingwa wa mikoa itakayofanyika baadaye.

“Niwapongeze wachezaji na makocha na uongozi wote wa benchi la ufundi kwa kweli mmeonesha kitu ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, kwa hiyo mjipange mkawakilishe mwaka huu tubebe ubingwa,”alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha soka la wanawake Somoe Ng’itu alisema awali walianza mashindano hayo kwa vituo vitatu ambapo walipata timu mbili kila kituo na awamu ya pili wakapata sita bora.
Alisema: “tunapenda kuwashukuru wadau wote na hasa DRFA kwa kutuunga mkono,”

Timu hizo tatu zilizofanikiwa kutinga tatu bora zitaiwakilisha mkoa wa Dar es Salaam kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa na pia, Ligi ya Wanawake ya daraja la kwanza.

Timu sita ndizo zilizofanikiwa kutinga sita bora ambazo ni Mbagala Queens, Rangi 3 Princess, Kinondoni Queens, Young Stars Queens, Safina Youth Soccer na Wisdom Queens.

Acha ujumbe