KARIAKOO DABI IMEINGILIWA NA WAZEE

MAMBO yameanza kuwa mengi kuelekea mchezo wa Simba na Yanga Jumamosi hii maarufu kama Kariakoo Dabi Ambapo kila upande Umefanyaa maandalizi ya utofauti.

Pande zote mbili, zimeukabidhi mchezo huo Kwa wazee wa timu hizo Ili ushindi Uweze kupatikana.kariakoo dabiAfisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema Kuelekea mchezo wao wa Kariakoo Dabi Jumamosi, Kila kitu wamekiacha kwenye mikono ya wazee wa timu hiyo.

Sambamba na upande wa Simba nao wamefanya kama Watani zao.

Kamwe alisema: “Hatuiangalii Simba kama nyie wengine mnavyoiangalia, sisi tunaingalia Simba kama timu Tishio na tunayowania nayo Ubingwa.

“Ni timu yenye wachezaji wazoefu na Viongozi wazuri na ndio maana sisi kama Young Africans SC haendi kwenye Derby kwa kuwaangalia Simba kama ambavyo waandishi na watu wengine wanavyoiangalia”

“Sisi kama Young Africans tumeamua mchezo huu wa Jumamosi tuwakabidhi Wazee wetu, huu mchezo wa Derby wa Jumamosi ni , Wazee wa Yanga wote hii mechi ni ya kwenu, tukifungwa ni nyie.

kariakoo dabi“Tunaomba mkatuheshimishe wazee wetu, mje kwa wingi Benjamin Mkapa lakini tunaamini pia kupitia Dua zenu tutafanya vizuri”

“Viingilio vya mchezo Kariakoo Dabi Jumamosi ni kama vifuatavyo;

VIP A – 50,000
VIP B – 30,000
VIP C – 20,000
MACHUNGWA – 10,000
MZUNGUKO – 5,000

Acha ujumbe