Kariakoo Dabi Iwe ya Kiungwana

ZIKIWA zimebaki takribani siku mbili kuelekea Kariakoo Dabi mchezo unasubiriwa kwa hamu sana na shauku kubwa na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, hatimaye unakaribia kufika Novemba 5 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Ni siku ya kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC, dhidi ya Simba SC, timu ambazo ni kongwe katika soka la nchini hii.kariakoo dabiUkiwa ni mchezo wa Kariakoo Dabi siku zote huwa na mambo mengi kuanzia ndani hadi nje ya uwanja, tunaomba amani itawale iwe mechi ya kiungwana.

Wale mashabiki wenye itikadi za kufanya fujo waache mara moja tunataka kuona burudani na sio vurugu.

Wachezaji nanyi kumbukeni soka ni mchezo wa kiungwana, hivyo msifanyiane zile rafu ambazo zitahatarisha afya ya mchezaji mwenzako.

Kuna maisha baada ya Kariakoo Dabi kikubwa lindaneni ndani ya uwanja ,mechi hii isivunje utu wenu.kariakoo dabiYote kwa yote tunazitakia kila la heri timu zote katika mchezo huo ambao umeteka hisia za wengi, mtoto atumwi dukani siku hiyo. Tanzania, Afrika na Dunia itakuwa inagazama ardhi ya Mswahili ikiwa inawaka moto.

Acha ujumbe