MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesisitiza kuwa mechi yao na Yanga inayochezwa kesho kutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa haitakuwa rahisi kwao kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Ahmed Ally amesema, Yanga wana wachezaji wengi hodari na wenye utimamu wa mwili na akili na wenye kukimbia muda wote ndani ya Uwanja. Hivyo wao kama Simba lazima waende kucheza kikubwa na kuonesha kuwa wao wakubwa zaidi ya timu zote Tanzania, ikwemo Yanga yenyewe.ahmed allyAhmed Ally alisema: “Mechi ya Simba na Yanga huwa ni mechi ngumu huwa haijalishi timu zote zipo kwenye hali gani. Hata mashabiki wa Simba tukicheza dhidi ya mashabiki wa Yanga unaona kabisa amsha amsha jinsi ilivyo.

“Hata kama Yanga awe vibaya kiasi gani wanaweza wakasafiri na lori kwenda mpaka Mbeya sababu ya kupitia hali ngumu lakini bado wakicheza dhidi yetu mechi huwa ni ngumu.

“Licha ya kufungwa na Ihefu ambayo imeshazoea kuwafunga Yanga, bado mechi yetu dhidi yao huwa ni mechi ngumu. Na ukiangalia mfululizo wa mechi zao kwasasa unaona kabisa itakuwa mechi ngumu.


“Wana wachezaji wazuri wenye uwezo wa kukimbia muda wote wa mchezo kwa maana ya dakika zote 90. Hii lazima niseme wazi, wapinzani wetu wana wachezaji wazuri sana.

“Lakini tutawafunga sababu sisi Simba tuna wachezaji wenye ubora kuliko wachezaji wao. Yanga wana wachezaji wenye ubora lakini ukiwalinganisha na wachezaji wa Simba, sisi ndiyo tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko wote.ahmed ally“Yanga wana wachezaji wenye ubora kuliko wa Azam, wa Azam wana ubora kuliko Mashujaa na sisi tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko hao wote, tuna wachezaji wenye ubora wa ngazi ya Afrika.

“Kama wachezaji wa Simba wakiamua mechi hii tunataka kushinda basi hakuna timu inaweza kutuzuia.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa