Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa, wanakwenda kuwatoa Al Ahly kwenye mechi yao ya African Footbal League. Ahmed ameyasema hayo leo kwenye mwendelezo wa hamasa Manzese Dar.
“Wale wengine Itawachukua si chini ya miaka 50 kutufikia tulipo na hatujaridhika, tunataka nafasi ya Al Ahly ya ubora barani Afrika kuwa namba moja na tutaichukua. Hakuna kinachoshindikana kwa Mnyama”“Dhamira yetu sio tu kumfunga Al Ahly, tumeshamfunga sana, safari hii tunataka kumtoa, na wamekuja wakati mbaya, wakati ambao tunataka sifa barani Afrika. Hatutamuacha salama”.Alisema Ahmed Ally
“Lazima tujidai kweli kweli, lazima tujivunie. Wakati sisi tunaangaika na timu namba moja Afrika wengine eti wanajidai na Dar Derby (Yanga vs Azam). Tunahangaika kumleta Infantino, Motsepe na viongozi wengine wakubwa. Tuna haki ya kujidai sana.”
“Yani CAF wakianzisha mashindano ya timu nne sisi tutakuwepo. Wengine kupata nafasi lazima mashindano yawe na timu 20 kwenda mbele. Hii ndio michuano yenye thamani zaidi barani Afrika na wenye michuano wakasema timu inayofanana na michuano hii Tanzania ni Simba Sports Club.”“Lazima tuambiane ukweli AFL ya safari hii imeshirikisha timu nane bora na Mnyama yupo kati ya timu hizo bora, AFL zijazo zitakusanya kila mtu ambayo haitakuwa na thamani sawa na hii ya kwanza.”alisema Ahmed Ally