KATIKA kuhakikisha wanafanikisha malengo ya kufuzu Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kamati ya Mashindano ya Yanga inaangalia uwezekano wa kuwaongezea bonasi wachezaji wake katika kila mchezo watakaoucheza katika hatua hiyo.
Timu hiyo, katika hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao waliwaondoa Al Merrikh ya nchini Sudan, mabosi hao waliwawekea bonasi ya Sh 250Mil ambazo walipewa wachezaji na Benchi la Ufundi la timu hiyo.Katika hatua hii ya makundi, Yanga wapo Kundi D, wakiwa na Al Ahly (Misri), CR Belouizdad (Algeria), Medeama FC (Ghana) na Yanga wenyewe wenye matumaini ya kufuzu hatua ya Rono Fainali kutokana na ubora wa kikosi chao kinachoongozwa na baadhi ya mastaa kama, Maxi Nzengeli na Stephene Aziz Ki.
Mmoja wa Mabosi wa Yanga, ameliambia gazeti la Championi Jumamosi, kuwa wanataka kuona hamasa na molari ya wachezaji inaongezeka, hivyo wamepanga kuwaongezea bonasi wachezaji wao ili malengo yafanikiwe msimu huu.Bosi huyo alisema kuwa bonasi hiyo huenda ikafikia Sh 300Mil, kwa kila mchezo watakaoupata ushindi wa nyumbani na ugenini itaongezeka na kufikia 350Mil ambayo atakabidhiwa nahodha.