KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa amefurahishwa na mabadiliko ya ratiba za ligi kuu ikiwemo mchezo wake na Azam FC utakaopigwa wikiendi hii.

Gamondi, amesema ratiba hiyo imekuwa rafiki na nzuri kwake kwani imempa nafasi ya kuwaambia wachezaji Djigui Diarra na Khalid Aucho kurudi haraka Bongo na kuingia kambini haraka, baada ya kumaliza majukumu ya kimataifa.AZAM“Nimefurahishwa na mabadiliko ya ratiba kwani nilikuwa naumiza kichwa namna ya kupata mechi ya kirafiki ili kuwajenga kimwili na kiushindani wachezaji wangu ambao wamekaa nje ya uwanja kwa muda bila mechi ya ushindani.

“Wachezaji wote wameshaingia kambini isipokuwa wale ambao waliitwa kwenye timu za taifa. Ni wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza wameitwa kwenye timu zao za taifa hilo haliondoi mimi kuendelea kuwaandaa wachezaji waliopo na wao pia wana mchango kwenye timu”

“Yanga haimtegemei mchezaji mmoja, wote wanategemeana hivyo kurudi kwa wachezaji ni mwanzo mzuri wa kuwaandaa tayari kwa ajili ya mchezo ulio mbele yetu, hautakuwa Mchezo rahisi tunakutana na timu ambayo haijapoteza Mchezo hata mmoja Azam FC, hicho ni kipimo sahihi cha mechi za ushindani,” – Miguel GamondiAZAM“Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho wanacheza mechi zao za mwisho za kirafiki, wakitumikia timu zao za taifa 18 Oktoba, nimewaambia warudi siku inayofuata Oktoba 19 ili kujiandaa na mchezo ulio mbele yetu.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa