MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Issa Masoud amefanya mahojiano na Egyptian TV Kujua wao kama Simba SC wamejiandaaje kwa maana ya maandalizi ya Ufunguzi pamoja na timu yao itakayocheza dhidi ya Al Ahly October 20, Benjamin Mkapa.
Kwenye mahojiano hayo Issa alisema wao kama Simba tayari wameshamalizana na maandalizi ya mchezo huo na kwa sasa wamejiandaa kufanya makubwa ikiwa malengo makubwa ni kushinda kwa mabao mengi.
Masoud alisema: “Timu inajiandaa vizuri na wachezaji wanaendelea na mazoezi na sisi kama Simba SC tunajua tunakutana na timu kubwa yenye historia kubwa Afrika, lakini tofauti na zamani, zamani ilikuwa ukikutana na timu kama Al Ahly mnakuwa wanyonge ila sasahivi imekuwa ni kinyume.
“Maana inakuwa kama hamasa au shauku kwasababu ni kipimo cha aina ya timu ambayo Simba SC inataka kuwa au mwelekeo huo, na tukio ni kubwa kwasababu lina sura ya kiafrika au kidunia kwa hivyo maandalizi yanakwenda vizuri katika ushirikiano wa serikali, CAF , FIFA na sisi Simba SC wenyewe”.Lakini pia Issa Masoud ameulizwa kuhusu Miquissone kuwa ataweza kufanya kama alichokifanya wakati ule na baadae kusajiliwa na Al Ahly?
Majibu ya Masoud yalikuwa: “Miquissone ni sehemu ya wachezaji waliosajiliwa na Simba SC, lakini pia ni mapendekezo ya kocha kuona anafaa kumtumia kwenye mchezo huo, lakini pia anaweza kufanya kama alichokifanya wakati ule kwasababu ni mchezaji mzuri na anaweza kufunga au kusababisha goli.”