UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa wapo ndani ya malengo yao katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya ligi ya Mabingwa barani Afrika ambapo malengo yalikuwa ni kuweza kutinga katika hatua ya makundi.
Yanga kwa sasa kwenye hatua hiyo ya makundi wamepangwa katika kundi D la michuano iyo sambamba na timu za CR Belouzdad kutoka Algeria, Al Ahly kutoka Misri na Medeama FC kutoka Ghana.Akizungumza na Championi Jumatano,
Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema wanashukuru kwa kuweza kufikia malengo yao ya kutinga makundi na kwamba watahakikisha wanapambana dhidi ya wapinzani ambao wamepangwa nao katika michuano hiyo ili wasonge mbele zaidi.
“Tunashukuru tumeweza kufikia malengo yetu katika michuano hii ya kimatifa,wakati msimu unaanza uongozi uliweka wazi kuwa malengo yetu msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika basi ni kuweza kuhakikisha kuwa tunafika kwanza katika hatua ya makundi.
“Tunashukuru tumefika na tayari tumewaona wapinzani wetu, sasa hatuwezi kuwasema kuwa kwa kuwa tayari tulishafikia malengo yetu basi ndio tusiende kupambana, hapana tumewaona wapinzani wetu ambo tumepangwa nao.“Ni wapinzani wazuri kwa maaana ni timu nzuri, kwanza ni mabingwa wote kutoka katika mataifa yao hivyo lazima tuwaheshimu kwa hilo lakini ni lazima tuhakikishe kuwa tunaweza kufanya kutafuta nafasi ya kwenda katika hatua inayofuata,” alisema Kamwe.