AHMED ALLY AFUNGUKA MIPANGO YAO

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally ameweka wazi juu ya mipango yao watakayotumia kuelekea kwenye mechi yao ya Jumapili.

Ahmed Ally alisema: “Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.ahmed ally“Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani.”

“Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi.”

“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui.”

“Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo.”

“Tarehe moja ya mwezi wa kumi ni siku ya Mnyama kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Sisi hatwendi kuweka historia, tunakwenda kwenye miasha yetu ya kawaida.”

“Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho hicho atakutana nacho. Bora wangekubali tukamalizana nao kwao.”

“Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi majira ya saa 12 jioni na shirika la ndege la ATCL. Waamuzi wanatarajia kufika Tanzania tarehe 30 Septemba.”ahmed ally“Huu mchezo CAF wanauangalia, wanaangalia timu ya CAF Football League. Itakuwa ni aibu eti timu ya CAF Football League alafu isiwepo hatua ya makundi.”Alisema Ahmed Ally

“Ule Uwanja ni wa Azam FC, Simba SC tutakwenda kucheza pale kutaka matokeo tu, amecheza nani, ameutumia nani hilo halitupi wasiwasi. Ule uwanja sio wa nyuma mwiko, sisi tutacheza na tutaingia hatua ya makundi. Wala mashabiki wasiwe na mashaka hata kidogo.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.