Tanzania, Kenya, na Uganda zimefanikiwa kushinda tena ya kuandaa michuano mikubwa inayohusisha mataifa nchini Afrika kupitia mpira wa miguu AFCON itakayofanyika mwaka 2027.
Tanzania na majirani zake kwa maana ya Kenya na Uganda wameingia kwenye historia kwa mara ya kwanza kuandaa michuano ya mataifa ya Afrika kwa upande wa wanaume mwaka 2027.Nchi hizi kutokea ukanda wa Afrika mashariki zinapata heshima hii chini ya uongozi wa Rais Patrice Motsepe kutoka Afrika Kusini, Ambapo Rais huyo ametangaza mchana huu kua mataifa hayo sasa yataandaa michuano hiyo mwaka 2027 kwa ushirikiano.
Hii inakua sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa michuano ya Afrika kwani wameshawahi kuandaa michuano ya Afrika katika ngazi ya vijana pamoja na wanawake, Lakini awamu hii wamefanikiwa kuandaa katika ngazi ya timu kubwa.Aidha Rais wa shirikisho la mpira Barani Patrice Motsepe amewapongeza marais wa nchi hizi tatu ambao ni Dkt Samia Suluhu Hassan, William Ruto wa Kenya, Yoweri Museni wa Uganda kwa kukubali kushiriki michuano hiyo mwaka 2027.