1: MTAZAMO WA KIUZALENDO
Simba wana nafasi ya kumfunga Al Ahly kwa mara nyengine tena katika dimba la Benjamin william Mkapa.
Kwanza Al Ahly wenyewe wamechoka sasa hivi hawajiwezi naamini anafungwa mechi zote mbili.
-Aliou Dieng sio yule, sasa hivi amechoka, unajua anatumika sana yule.
2:MTAZAMO WA KIUHALISIA.
Uhalisia wa mchezo huu kati ya Simba dhidi ya Ahly ni kwamba hizi timu mbili mpaka sasa hakuna anayeonekana ana nafasi ya kuendelea kumzidi mwenzie.
-Mara kwa mara Simba na Ahly wamekutana na wameonyeshana ubabe hivyo mpaka sasa hakuna mwenye nafasi kubwa sana kumliko mwenzake.-Mchezo huu nauona kabisa ni 50% – 50% kati ya timu zote mbili hizo inawezekana bingwa wa mchezo huo akapatikana kwa mikwaju ya penati pia.