Yanga SC imetwaa taji la 3 mfululizo la Kombbe la Shirikisho lakini ni kama bado wana kinyongo na aliyekuwa mchezaji wao zamani, Feisal Abdallah Salum, Feitoto. Kwani mchezo ulivyomalizika kupitia ukurasa wa klabu hiyo waliposti picha ya kombe lakini kwa mbali alionekana vizuri zaidi Feitoto akipita kwa machungu ya kupoteza mchezo. Beti na Meridianbet kwa Odds kubwa na Michezo ya Kasino ya Mtandaoni.
Picha hiyo ilisindikwa na Ujumbe uliosemeka “KAMA NANENO NI MKUKI” Hapa wakaachiwa mashabiki na wadau kumalizia majibu, picha hii imezua gumzo mitandaoni kila mtu akitoa maoni yake.
Feitoto alikuwa na kiwango bora sana kwenye mchezo huo wa fainali, alipokuwa akienda kupiga penati mashabiki wa Yanga walikuwa wakimzomea, lakini alipiga na kufunga ile penati ndipo alipowageukiwa na kuwafunga midomo.
Akitokea nje ya uwanja alikokaa miezi 8 bila kucheza mchezo wowote wa kimashindano; Feisal Salum Abdallah anapata takwimu hizi ndani ya msimu 2023/24
-Magoli 19
-Asissts 7
-Nafasi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 anaipeleka Azam FC
– Fainali ya CRDB FA Cup
– AFCON hatua ya makundi kwa mara ya pili (2019&2023)