Yanga Baba Lao! Ubingwa wa 8 FA, Simba Kaachwa Mbali Sana

Yanga Baba Lao! Kuna Jingine huko Wananchi wanauliza baada ya usiku wa kuamkia leo Juni 3, 2024 kuibuka mabingwa wa Kombe la Shirkisho, hii ni mara ya 8 Yanga anachukua Kombe hili tangu lianzishwe mwaka 1967 likiwa na jina la Kombe la FAT.

 

yanga sc
Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto akiwa amesujudu ishara ya kushukukuru mafanikio yake na ya kalbu kwa Msimu 2023/24. Picha hii imepigwa June 2, 2024 baada ya klabu hiyo kutwaa Taji la 8 la Kombe la Shirikisho.

Tangu kurejea tena kwa mashindano hayo mwaka 2015, Yanga wamefanikiwa kulibeba kombe hilo mara 4, ikizidisha Simba na Azam FC ambao kwa upande wa Mnyama yeye amechukua mara 4 tu kuanzia mwaka 1967, Simba kachukua ubingwa wa FA mara 4 (1995, 2016/17, 2019/20, 2020/21).

MABINGWA WENGINE WA KOMBE LA SHIRIKISHO

Yanga SC kachukua mara 7 kuanzia mwaka, 1967,1974,1999,2001,2015/16,, 2021/22, 2022/23, 2023/24. Bashiri na Meridianbet kuwa Milionea mkubwa! Ushindi upo hapa.

Azam FC wao wamechukua ubingwa huo mara moja tu mwaka 2018/18.

Timu zingine zilizowahi kuchukua ubingwa wa FA, Majimaji ya Songea 1985, Sigara FC, 1996, Tanzania Stars 1997, 1998, Mtibwa Sugar 2000, JKT Ruvu 2002, 2003-2015 Haikuchezwa, 2017/18

JINSI FAINALI ILIVYOKUWA

Siku ilitaka kuwa mbaya kwa Yanga ambao walianza kwa kukosa mikwaju miwili ya penati, Aziz Ki na Joseph Guede walikosa penati za mwanzoni, lakini Diarra aliwarudisha mchezoni.

Makocha wa timu zote mbili walizingumzia mchezo wenyewe huku Gamondi akitoa pongezi zaidi kwa wachezaji wake.

β€œLeo tulikuwa vizuri, kipindi cha kwanza timu ilitengeneza nafasi lakini hatukuweza kuzitumia, kipindi cha pili Azam FC walijaribu kuwa nyuma na kipa wao kupoteza muda lakini tumeshinda kwa mikwaju ya penati”

β€œKwa wachezaji na benchi la UFUNDI tunatakiwa kuamini hadi mwisho wa mchezo, haijalishi tulikosa penati mbili lakini tulikuwa tunaamini tunaweza kuchukua ubingwa” Muguel Gamondi.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Azam FC, Yusuf Dabo alielezea hisia zake baada ya kupoteza ubingwa huo ambao ungekuwa wa pili kwao tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 1967.

β€œWapinzani walipoteza mikwaju miwili, na sisi hatukuweza kuzitumia hizi nafasi kumaliza mchezo, niwapongeze wachezaji leo tulikuwa bora lakini tumekuja kupoteza kwenye penati, hazina mwenyewe” Kocha Msaidizi wa Azam FC Yusuf Dabo.

Mchezaji bora wa mashindano hayo alikuwa ni Ibrahim Bacca, ambapo alisema haya baada ya mchezo kumalizika.

” Ilikuwa ni mechi nzuri, lakini kwa uimara wetu na ubora wetu tumeweza kutetea ubingwa huu” Ibrahim Bacca Mchezaji bira wa mchezo. Tuliweza kupambana dakika 120 lakini tulienda kwenye mikwaju ya penati ambayo haina mwenyewe, na Yanga wamechukua”

β€œKwa siku kama ya leo kipa alicheza penati mbili lakini timu tukashindwa kutumia nafasi, nimpe polee kipa wetu (Mustafa Mohamed) kwa kukosa kombe” Lusajo Mwaikenda.

 

Acha ujumbe