YANGA WAWATEGA AZAM FAINALI FA

 

KUELEKEA katika mchezo wa fainali ya CRDB Federation Cup leo Juni 2 2024 kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, mabingwa watetezi YANGA wamedai kuwa hawana kisasi chochote Kwa Azam FC na watacheza mechi hiyo kama wapo mazoezini.

Wananchi ni mabingwa watetezi wa taji hilo wakilitwaa Msimu uliopita mbele ya Azam FC na wanakumbuka walipokutana na Azam FC katika mchezo wa ligi mzunguko wa pili walipotoza kwa kufungwa mabao 2-1.yangaMiguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wao utakuwa na ushindani mkubwa ila watapambana kucheza soka safi hawafikirii kuhusu kulipa kisasi.

“Yanga ndiyo timu inayocheza soka safi zaidi Tanzania hilo lipo wazi lakini kuelekea mchezo wetu wa fainali tupo vizuri na hatuna mpango wa kulipa kisasi kwa kuwa mchezo wa mpira hauhitaji kulipizana visasi bali maandalizi.

“Ninaamini kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa hilo lipo wazi tutafanya kazi kubwa kwa kuwa wachezaji wapo tayari hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.”.yangaMwamuzi wa mchezo huo wa fainali ni Ahmed Arajiga ambaye alikuwa pia ni mwamuzi kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Acha ujumbe