AZAM FC YAITOLEA YANGA KAULI YA KIBABE

AZAM FC wapo tayari Zanzibar kwa vita ya mwisho ya msimu kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya Yanga.

Ni CRDB Cup inatarajiwa kuchezwa leo Juni 2 2024 Uwanja wa New Amaan Complex, Baada ya Uongozi kusema wanautaka mchezo huo.azam fcUongozi na wachezaji wa timu hiyo wamesema kuwa hii ni karata muhimu zaidi kwao ya kuhakikisha wanaumaliza msimu wakiwa na taji mkononi na hivyo watapambana kufa na kupona.

Ikumbukwe kwamba Azam FC kwenye fainali ya 2022/23 walipoteza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kushuhudia ubao ukisoma Azam FC 0-1 Yanga na bao pakee la ushindi lilifungwa na Kennedy Musonda.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameweka wazi kuwa wanachukulia fainali kwa umakini na wanatambua umuhimu wa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao.azam fc“Tuliweka wazi tangu awali kwamba tunahitaji kufanya vizuri hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa fainali.”

Acha ujumbe