AZAM FC WANAUTAKA UBINGWA

AZAM FC wapo tayari Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya Yanga.

Ni CRDB Cup inatarajiwa kuchezwa Junj 3 2024 Uwanja wa New Amaan Complex kwa kila timu kupambania taji hilo.azam fc

Miongoni mwa wachezaji waliopo na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo ni pamoja na Feisal Salum, Jhonier Blanco ambaye ni mshambuliaji mpya wa Azam FC.

Ikumbukwe kwamba Azam FC kwenye fainali ya 2022/23 walipoteza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kushuhudia ubao ukisoma Azam FC 0-1 Yanga na bao pakee la ushindi lilifungwa na Kennedy Musonda.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameweka wazi kuwa wanachukulia fainali kwa umakini na wanatambua umuhimu wa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao.azam fc“Tuliweka wazi tangu awali kwamba tunahitaji kufanya vizuri hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa fainali.”

Acha ujumbe