Ulikuwa msimu bora sana wenye ushindani mkubwa ndani na nje ya uwanja, kila timu imechukua kadi yake stahiki kutoka Ligi kuu ya NBC 23/24 kwa walivyojipanga mwanzo mwa msimu mpaka mwisho.
Hongera sana Yanga kuibuka bingwa kwa msimu huu watatu mfululizo hakuna bahati yoyote ile,ni maandalizi bora kutoka kwa viongozi, benchi la ufundi na juhudi za wachezaji uwanjani, point 80 ni nyingi mno kuibuka bingwa kabla ya michezo mitatu sio kitu kidogo, kama mashabiki wamejivumia na kutamba mtaani kwa mafanikio tukutane mwakani tena na CAFCL.Hongera sana Azam fc ligi haikuwa nyepesi kwenu kama ambayo ZakaZakazi alisema malengo yenu ni kutengeneza timu bora zaidi ili baada ya miaka mitatu kuweza kuwa tishio zaidi, kila kitu na hatua ya kwanza ni kumaliza nafasi ya pili msimu kwa point 70 ambazo zimetosha msimu ujao kushiriki CAFCL ni kitu kikubwa sana kwenu, pongezi kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kijumla.
Hongera sana Simba huenda hayakuwa malengo ila ndio uhalisia wenyewe wa mpira mguu aliyebora ndiye ushinda mechi,ni wakati mzuri sana wa kutumia busara kutengeneza timu mpya yenye ushindani, hamjapoteza kabisa ni kujikwa kumaliza nafasi ya tatu na point 70, bado nafasi ipo mwakani ya kimataifa kushiriki CAFCC… msimu ulikuwa mgumu kwenu kuondoka kwa makocha ila ndio mchezo wa mpira, pongezi Kwa Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wote.
Hongera sana Wagosi wakaya mlisema mwanzo mwa ligi kimataifa msimu ujao ni yenu na imekuwa kweli, mmpembana sana ligi kuu haikuwa nyepesi kihivyo umejitoa Kwa moja wenu mpaka mwisho mwa msimu, kuwa nafasi ya nne kwa points 44 ni kitu kikubwa lazima maandalizi yalikuwa madhubuti kweli kweli…wasas ni wenu karibuni kimataifa msimu ujao CAFCC.Asante sana Mtibwa Sugar una historia na soka ili kwa kutoa vipaji vingi vya kutosha sana miaka 25;+ kuwepo kwenye ligi ni jambo la kishuja ila kwa sasa nyakati zimeamua yupo anastahili kubakia ligi kuu NBC. Kwa Kheri na karibu sana Championship msimu ujao.
Asante sana Geita Gold imeniuma kuondoka ligi kuu ya NBC kabla ya kuona ukiwa unatumia uwanja wako…kila safari ina mwanzo na mwisho basi tuseme leo ndio umekuwa mwisho wako kupiga stori tukiwa ligi kuu NBC, kwa Kheri na karibu sana Championship msimu ujao.