BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia leo ameshinda Ubingwa wa WBO kwa TKO ya raundi ya pili kwa kumpiga Bondia Mghana Patrick Allotey kwenye Ukumbi wa Warehouse uliopo Masaki, Dar es Salaam.
Allortey alishindwa kuendelea na pambano hilo kwenye raundi hiyo ya pili akidai kuwa ameumia bega na hawezi tena kuendelea na mchezo huo.Pambano hilo lilipangwa kuchezwa June 01, 2024, lakini lilishindwa kufanyika kwasababu mwakilishi wa WBO Afrika, Samir Captain kutoka nchini Ghana kushindwa kufika ukumbini.
Mwakinyo alisema sababu iliyokwamisha pambano hilo mbele ya mashabiki: “Kuna changamoto kidogo imejitokeza, inabidi pambano letu sisi lisimamiwe na rais wa WBO ambaye yupo Dar es salaam lakini kuna changamoto zilitokea katika utafutaji wa malipo yake kutokana na changamoto ya kupatikana kwa Dola.“Mzee ametafutwa na hapatikani kwenye simu, kwa upande wetu tumejiandaa vya kutosha na tuna utayari wa kupigana lakini kinachoweka uzito ni hicho, nina hamu ya kukata kiu ya mashabiki wangu lakini nikifanya hivyo ni makosa na itaharibu kabisa carrier yangu” Alisema Mwakinyo.