Kampuni ya PAF Promotion imemfungulia shauri la Madai Bondia Hassan Mwakinyo ambalo linatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 13, 2023 katika Mahakama ya Kisutu.

Baadhi ya madai yanamtaka Mwakinyo aombe radhi kwa kugoma kupanda ulingoni Septemba 29, 2023 na kutoa taarifa za uongo kupitia Vyombo vya Habari.MWAKINYOMengine ni kulipa fidia Tsh. Milioni 142.5 (hasara ya kukosa mapato), kurejesha Tsh. Milioni 7.4 alizopokea, kulipa Tsh. Milioni 8 (gharama ya ukumbi), Tsh. Milioni 1.2 (malazi ya bondia mpinzani), Tsh. Milioni 3.8 (gharama za tiketi za ndege za mpinzani na wasaidizi wake) na faini ya Tsh. Milioni 150 (madhara ya jumla).


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa