Bondia kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo amefungiwa mwaka mmoja kushiriki mchezo huo baada ya kugomea kupanda ulingoni katika pambano lake lililopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi Septemba.
Mwakinyo amefungiwa mwaka mmoja kutoshiriki mchezo wa ngumi na faini ya milioni moja kutoka kwa kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania inayofahamika kama (TPBRC).Bondia huyo alitakiwa kupanda ulingoni tarehe 29 mwezi Septemba na mpinzani wake Julias Indongo kutoka nchini Kenya, Lakini alikataa kushiriki pambano hilo kwa kile alichodai kuvunjwa kwa makubaliano baina yake na waandazi wa pambano hilo.
Bondia Hassan Mwakinyo kutoka mkoani Tanga alieleza kua waandazi wa pambano hilo walikiuka makubaliano waliyokubaliana, Kwani waliwajumuisha wadhamini ambao bondia huyo hakuwataka na ndio ilikua sababu kubwa ya kukata kupanda ulingoni usiku wa tarehe 29 Septemba.
Kamisheni inayosimamia ngumi za kulipwa pia iliongeza kua adhabu hiyo haikuishia kwa bondia Hassan Mwakinyo kukataa kupanda ulingoni, Lakini pia ilitokana na maneno machafu mbele ya kamati iliyokua ikisikiliza shauri lake.