Bondia wa kitanzania Hassan Mwakinyo, amefungiwa kutojihusisha na mchezo wa ngumi nchini taarifa iliyotolewa mapema na mamlaka za mchezo nchini humo.

Chama kinachosimamia wanaopigana ngumi za kulipwa nchini humo kinachojulikana kama BBBC, kimetoa taarifa hiyo sababu za kufungiwa kwa bondia huyo zikiwa bado hazijawekwa wazi.

mwakinyoHii imekuja baada ya kupigana na bondia wa nchini humo Liam Smith, na kupoteza kwa TKO raundi ya nne tu ya mchezo, pambano ambalo liliacha maswali mengi sana kwa wapenzi wa mchezo huo.

Hali hii haitamuathiri bondia huyo namba moja kwa ubora nchini, kwani ataweza kuendelea na shughuli zake za ngumi katika nchi nyingine isipokua nchini Uingereza, hali ambayo imeshamkuta bondia Liam Smith ambae alifungiwa kushiriki mchezo huo nchini Marekani.

Kutokana na kufungiwa kwa Mwakinyo, hii inaonesha wazi kua pambano la marudiano baina yake na Liam Smith lililopangwa kuchezwa tena halitarudiwa nchini humo bali katika nchi nyingine kabisa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa