Uingereza Kuandaa Euro2028

Uingereza pamoja na washirika wake wataandaa michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2028 hii ni baada ya kufanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha kuandaa michuano hiyo.

Shirikisho la soka ulaya UEFA limetangaza kua mataifa ya Uingereza, Wales,Scotland, na Jamhuri ya Ireland zitaandaa michuano ya EURO mwaka 2028 na michuano hiyo itapigwa katika mataifa manne.UingerezaMichuano ya Euro 2024 itapigwa nchini Ujerumani mwakani ambao walifanikiwa kushinda tenda ya kuandaa michuano hiyo mbele ya mataifa mengine ambayo yalikua yanagombania tenda hiyo kama ilivyo kwa Uingereza na washirika wake.

Imewekwa wazi maeneo ambayo viwanja vyake vitatumika katika michuano ya Euro 2028 ambayo ni Belfast, Birmingham, Cardiff, Dublin, Glasgow, Liverpool, London (x2) Manchester na Newcastle.

 

Acha ujumbe