Mshambuliaji wa klabu ya Berntford Ivan Toney ameitwa kikosi cha timu ya tifa ya Uingereza ambacho kitakwenda kucheza michezo ya kuwania kufuzu michuano ya Euro ambayo inatarajiwa kufanyika mwakani.
Mchezaji Ivan Toney amefanikiwa kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kutokana na kiwango ambacho amekua akionesha ndani ya klabu ya Brentford, Huku akiiwezesha klabu hiyo kua moja ya vilabu kumi bora ndani ya ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa.Mshambuliaji huyo amekua na ubora mkubwa kwani mshambuliaji mmoja tu wa kiingereza ambaye anamzidi kupachika mabao ambaye ni Harry Kane, Lakini washambuliaji wote kutoka nchini Uingereza wako nyuma ya mshambuliaji huyo kwenye upachikaji wa mabao.
Kocha Gareth Southgate ameamua kumuita mchezaji huyo kwenye kikosi chake baada ya kuridhishwa na kiwango chake ambacho anakionesha mpaka wakati huu, Lakini pia wadau mbalimbali wanaamini mshambuliaji huyo alistahili kuitwa pia kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana. Kocha Southgate alipokea lawama nyingi baada ya kumuacha Ivan Toney kwenye kikosi chake cha mwisho kilichoelekea nchini Qatar kwajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka jana, Kwani wengi waliamini mshambuliaji huyo alistahili kuitwa lakini hatimae mchezaji huyo ameweza kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu hiyo.