Winga klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Raheem Sterling ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kilichoitwa na kocha wa timu hiyo Gareth Southgate kuelekea michezo inayofuata.
Winga Raheem Sterling ambaye alikua anaonekana kama mchezaji kipenzi cha kocha Gareth Southgate lakini wakati huu ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, Mchezaji huyo amekua hayupo kwenye kiwango kizuri tangu atimkie klabu ya Chelsea.Kocha Gareth Southgate amezungumza juu ya kumuacha winga huyo ambaye amekua muhimu kwenye kikosi chake kwa muda mrefu na kusema kiungo huyo hayuko fiti na kusema ndio sababu ya kutomuita, Lakini akasema kama mchezaji huyo angekua fiti angemuita.
Raheem Sterling hajakua kwenye kiwango kizuri sana ndani ya Chelsea na inaweza kua sababu kubwa ya kuachwa kikosi cha kocha Gareth Southgate, Kocha huyo ameonesha bado anaamini kwenye uwezo wa kiungo huyo kwani akirudi kwenye uboea au kua fiti ataitwa kwenye kikosi cha timu hiyo.Wachezaji wengine kadhaa wametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza mbali na winga Sterling ikiwemo beki Trent Alexender Arnold kutoka Liverpool na beki wa klabu ya Arsenal Ben White wote wakiwa mabeki wa kulia kwenye vilabu vyao, Sababu ya kuachwa kwao inaelezwa ni kocha kutokuridhidshwa na mwenendo wao.