Manchester United Kumaliza Kazi Leo?

Klabu ya Manchester United itakua ugenini leo kukabiliana na klabu ya Real Betis katika mchezo wa marudiano kombe la Europe league hatua ya 16 bora ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford ulimalizika kwa Man United kushinda 4-1.

Manchester United leo watacheza mchezo wa marudiano katika dimba la Benito Villamarin ambapo wataangalia namna ya kuweza kumaliza kazi waliyoianza wakiwa nyumbani wiki iliyomalizika, Klabu hiyo ina mtaji wa mabao matatu mpaka sasa ambao una faida kwa upande.manchester UnitedVjana hao wa Erik Ten Hag watakwenda kwenye mchezo huo wakiwa hawajafanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika michezo yao miwili ya ligi kuu ya Uingereza ambapo walipoteza mmoja na kusuluhu mmoja, Hivo hii inaweza ikawa sio ushara nzuri kwao kuelekea mchezo huu.

Klabu ya Real Betis wao chini ya kocha Manuel Pellegrini watakua na kibarua cha kuhakikisha wanapindua meza katika dimba lao la nyumbani baada ya kukubali kichapo kizito ugenini wiki iliyomalizika, Hivo watahakikisha wanaweza kupata matokeo leo dhidi ya Manchester United.manchester UnitedKlabu ya Manchester United leo itawakosa nyota wake kadhaa ambao wamepata majeraha kama kinda Alejandro Garnacho ambaye ameumia wikiendi iliyomalizika katika mchezo dhidi ya Southhampton, pamoja winga wa Brazil Antony ambaye kocha Ten Hag amethibitisha hatakuepo baada ya kuumia.

Acha ujumbe