Horoya Yatua Dar es salaam Kwaajili ya Kukipiga Dhidi ya Mnyama Kesho

Timu ya Horoya imetua hii leo jijini Dar es salaam kwaajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku katika Dimba la Benjamin Mkapa.

 

Horoya Yatua Dar es salaam Kwaajili ya Kukipiga Dhidi ya Mnyama Kesho

Ikumbukwe kuwa timu hizi mbili, Horoya na Simba zote zinatafuta pointi tatu kwaajili ya kuhakikisha wanavuka na kwenda hatua ya robo fainali kwenye michuano hii ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Mechi ya kwanza Simba alipoteza akiwa ugenini kwa bao 1-0 huku wakishindwa kutumia nafasi za wazi ambazo walikuwa wamezipata na kufanya wadondoshe alama kwenye mchezo wao wa kwanza.

Horoya Yatua Dar es salaam Kwaajili ya Kukipiga Dhidi ya Mnyama Kesho

Lakini licha ya Simba kupoteza dhidi ya Horoya, bado anashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo akiwa na alama sita baada ya kushinda mechi zake mbili huku mgeni yeye akiwa nafasi ya tatu na pointi zake nne mpaka sasa.

Simba wana matuamini ya kwenda robo fainali ya michuano hii, halikadhalika kwa upande wa mgeni naye. Je Robertinho na vijana wake watafanya nini hapo kesho kupata matokeo ambayo wana Msimbazi wanatarajia.

 

 

Acha ujumbe