Afisa Habari wa klabu Simba Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wao Augustine Okra na Ismail Sawadogo wataukosa mchezo wao watakaocheza dhidi ya Horoya siku ya Jumamosi tarehe 18.

 

Okra na Sawadogo Kuwakosa Horoya Machi 18

Okra alivunjika kidole kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Al Hilal na alitarajiwa kuwa nje kwa wiki nne lakini sasa bado ataendelea kuwa nje huku akifanya mazoezi kidogo dogo. Lakini Kibu Denis yeye amerejea na atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Horoya.

Mchezo huo ni wa klabu Bingwa ambapo mechi ya kwanza walipokutana Simba alipoteza kwa bao 1-0 na mechi hii mnyama anahitaji ushindi ili ajihakikishie nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Vijana wa Robertino wapo nafasi ya pili kwenye kundi wakiwa na pointi 6 huku anayeongoza kundi akiwa ni Raja Casablanca mwenye pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote nne.

Okra na Sawadogo Kuwakosa Horoya Machi 18

Horoya yupo nafasi ya tatu akiwa na pointi nne na pia bado ana matumaini ya kusonga mbele endapo akishinda michezo yake miwili iliyopita, hivyo ni mechi ya kufa na kupona ndani ya Benjamin Mkapa kila timu inahitaji ushindi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa