Klabu ya US Monastir yatua jijini Dar es salaam hii leo kwaajili ya mchezo wao wa siku ya Jumapili wa Kombe la Shirkisho dhidi ya Yanga.

 

US Monastir Yatua Dar es salaam Tayari kwa Kuwavaa Yanga

Mchezo huo utapigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 kamili usiku huku Yanga akihitaji ushindi wa alama tatu kwani anashikilia nafasi ya pili kwenye kundi hilo akiwa na pointi 7 huku Monastir wakiwa nazo 10.

Mechi ya kwanza walipokutana Yanga alipoteza kwa mabao 2-0 akiwa ugenini, huku mabao yote ambayo yalifungwa yakiwa ni ya mipira ya kutenga baada ya hapo akashinda mechi zake mbili na sare moja.

US Monastir Yatua Dar es salaam Tayari kwa Kuwavaa Yanga

US Monastir anahitaji pointi tatu ili aendelee kushikilia nafasi ya kwanza, lakini pia mwenyeji naye anahitaji hizo hizo pointi tatu. Sasa nani anaweza kuwa mbabe kwa mwenzake hii leo huku Wananchi wakitaka kulipa kisasi?

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa