Mabondia wanawake wanaoiwakilisha Tanzania kwa mara ya kwanza katika mashindano ya 13 ya Ubingwa wa Dunia (IBA) wameendelea na mazoezi mepesi jana jioni kujiweka sawa kwa mapambano yao.

 

Beatrice na Rahma Waendelea na Mazoezi Mepesi

Leo Ijumaa 17-03-2023, saa 9.30 alasiri muda wa Tanzania Nahodha wa timu Beatrice Ambros Nyambega ataandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza mwanamke kupigana katika mashindano makubwa na ya Ubingwa wa Dunia yaliyoanzishwa mwaka 2001, Scranton  Marekani.

Beatrice atapambana na Jasmine ambaye ni mwenyeji wa India katika bout no.55 , uzani wa lightweight 60kg .

Beatrice na Rahma Waendelea na Mazoezi Mepesi

Siku ya kesho Jumamosi bondia Rahma Joseph Maganga amabye anavalia jezi ya blue atapambana na Christine Ongare kutoka Kenya katika bout no. 72, uzani wa minimum weight 48kg.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa