Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Chelsea Raheem Sterling anatarajiwa kurejea kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza kuelekea mchezo wa robo fainali wa kombe la dunia dhidi ya Ufaransa.

Mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Chelsea alisafiri kuifata familia yake baada ya kuvamiwa na kuibiwa vitu vya thamani, Hivo ikampasa staa huyo kusafiri hadi nyumbani ili kuhakikisha familia yake inakua salama.sterlingSterling alikosekana kwenye kikosi cha kocha Gareth Southgate kilichofanikiwa kuibamiz timu ya taifa ya Senegal kwa mabao matatu kwa moja kwenye mchezo wa 16 bora na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.

Shirikisho la soka nchini Uingereza limesema staa huyo anatarajiwa kurudi na kujiunga na timu hiyo kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi.sterlingRaheem Sterling anatarajiwa kutokuanza kwenye mchezo huo wa robo fainali siku ya Jumamosi baada ya kukosa vioindi kadhaa vya mazoezi, Hivo kufanya kua na ufinyu wa nafasi katika mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa