Kocha wa klabu Napoli vinara wa ligi kuu ya Italia Luciano Spalletti amepingana na kauli ya kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola kua klabu ya Napoli ndio klabu bora kwasasa barani ulaya.

Kocha Spalletti anaamini kauli ya Pep Guardiola ipo kwajili ya kuwazuga ili waweze kuwaangusha na kocha huyo amesema hakubaliani na kauli kwakua anajua huo ni mchezo ambao kocha huyo wa kimataifa wa Hispania anawachezea na amegundua.spallettiKlabu ya Napoli imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuwatoa Eintracht Frankfurt kwa jumla ya mabao matano kwa bila hapo jana, Hivo kuwafanya vinara hao wa ligi kuu ya Italia Serie kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

Kocha Spaletti baada ya kuisaidia timu yake ya Napoli kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya aliulizwa kuhusu kauli ya Guardiola na kusema “Sijiskii Fahari, sijiskii chochote naujua mchezo huu ambao kila mtu anataka kuweka shinikizo kwa wengine, Unaiweka Napoli mbele ya City ambayo inaweza kutumia €900 milioni ukilinganisha na sisi tunaotumia €9milioni lazima kuwe na sababu ni mchezo wa kutaka kutuangusha”spallettiKocha Spalletti anajivunia kuifanikisha Napoli kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza na yeye kua sehemu ya historia, Lakini akipinga vikali sifa walizomwagiwa na kocha wa Manchester Pep Guardiola huku yeye akiona kama ni mchezo wa akili anaoucheza kocha huyo ili kuwaangusha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa