Leo Jumatano Kamati ya Utendaji ya Yanga chini ya Rais Eng Hersi Said imekaa kikao cha pili cha kikatiba kwa mwaka 2023 kujadili mambo mbalimbali yahusiyo klabu hiyo.

Kikao hicho cha viongozi wa Yanga kilijadili mambo mengi pamoja na kuweka mipango na mikakati ya namna wanaweza kuutwaa tena ubingwa wa ligi kuu pamoja na kufanya vizuri kwenye CAF Champions League.

Inaelezwa pia Leo huenda Rais wa Yanga SC, Eng Hersi Said akawaeleza wajumbe dhamira ya CAF pamoja na FIFA ya kutaka Yanga SC kushiriki mashindano yajayo ya Africain Football League.YANGADhamira ambayo FIFA kupitia kwa Rais wake Gianni Infantino na kwa CAF kupitia kwa Rais wake Patrice Motsepe wamemueleza kuwa Yanga SC lazima iwepo mashindano yajayo ya AFL.

Yanga SC msimu huu dhamira yao ni kutetea ubingwa na kufanya vizuri CAFCJIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa