Kiungo wa timu ya taifa ya Italia anayekipiga kwa klabu ya Newcastle United Sandro Tonali huenda akafungiwa miezi kumi ya kutojihusisha na mchezo wa soka kutokana na skendo ya kujihusisha na kucheza kamari.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia alituhumiwa wiki moja nyuma kujihusisha na michezo ya kamari na mamlaka nchini Italia, Huku taarifa zikieleza kua imethibitika mchezaji huyo amejihusisha na michezo ya kamari.Kiungo Sandro Tonali kwasasa anasubiri taarifa rasmi ya mamlaka inayoshughulika na michezo ya kubashiri, Hii inatokana na vielelezo kujitosheleza kua mchezaji huyo amejihusisha na michezo ya kamari
Klabu ya Newcastle United inatarajia kumkosa kiungo huyo raia wa kimataifa wa Italia kwa miezi kumi ambayo atakua nje ya uwanja, Jambo ambalo litakua pengo kwa klabu hiyo.Sandro Tonali alikua na mchezaji mwingine Nicolo Zaniolo katika tuhuma hiyo ya kujihusisha na michezo ya kamari, Lakini mpaka sasa taarifa zinaeleza kua mchezaji huyo ndio amekutwa na hatia.