Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Rodrygo Goes ameweka wazi kua hana mpango wa kutimka ndani ya klabu hiyo licha ya kuhusishwa kuondoka ndani ya timu hiyo.
Baada ya kushinda taji la ulaya jana Rodrygo aliulizwa juu ys mustakabali wake ndani ya klabu ya Real Madrid na kuweka wazi kua hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo na ataendelea kusalia sana klabunu hapo.Real Madrid wameshamalizana na winga wa zamani wa klabu ya PSG Kylian Mbappe jambo ambalo linawafanya wengi kuamini ni muda sahihi wa winga huyo wa kimataifa wa Brazil kutimka klabuni hapo, Lakini mchezaji huyo ameweka wazi hana mpango wa kuondoka ndani ya timu hiyo licha ya ujio wa Mbappe.
Winga huyo alisaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid ambao utamuweka klabunmi hapo mpaka mwaka 2028,Huku akisisitiza ana furaha ndani ya timu hiyo na ataendelea kutumikia mkataba wake.Winga Rodrygo aliulizwa juu ya kuhusishwa na klabu ya Manchester City lakini yeye ameeleza hatambui chochote juu ya tetesi hiyo, Lakini pia hatakama ni kweli kuna maombi yametumwa hayuko tayari kwani yeye akili yake ameiweka ndani ya Real Madrid.