Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Rodrygo Goes amesema hawezi kwenda kucheza ligi kuu ya Saudia maarufu kama Saudi Pro League.
Rodrygo amesema hajapokea ofa yeyote kutoka kwenye klabu yeyote inayoshiriki ligi kuu ya Saudia na taarifa hizo ni za uongo, Mchezaji huyo amekanusha hayo akiongea na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wao wa timu ya taifa.Mchezaji huyo ameweka wazi kua kwasasa anafikiria kuitumikia klabu ya Real Madrid tu na akili yake haiwazi sehemu nyingine yeyote, Kwakua anaipenda klabu hiyo na kila kitu kipo sawa klabuni hapo.
Ni wazi kua mchezaji huyo ni ngumu kuenda kucheza ligi kuu ya Saudia Arabia kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri wake, Lakini pia ni moja ya wachezaji waliopo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.Mshambuliaji Rodrygo tarehe 2 mwezi huu wa kumi na moja alifanikiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2028, Hii inaonesha kwa namna gani klabu hiyo ina mipango na mchezaji huyo na ni wazi hawezi kuelekea Saudia Arabia.