Bellingham Mchezaji wa Nne wa Madrid Kushinda Taji Nyumbani

Kiungo wa klabu Real Madrid Jude Bellingham ameingia kwenye rekodi ya wachezaji wa Real Madrid kushinda taji kwenye ardhi yake ya nyumbani baada ya jana kushinda taji la mabingwa ulaya jana usiku.

Bellingham anakua mchezaji wa nne wa Real Madrid kushinda taji la ulaya kwenye ardhi yake ya nyumbani na hii ni baada ya watangulizi wake kufanya hivo kama Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale.bellinghamCristiano Ronaldo alifanikiwa kushinda taji la ulaya mwaka 2014 katika jiji la Lisbon nchini kwao Ureno, Mwaka 2017 Gareth Bale alishinda taji katika jiji la Cardiff nchini kwao Wales, Karim Benzema alifanikiwa kushinda taji la ulaya pia mwaka 2022 jiji Paris nchini kwao Ufaransa.

Bellingham anaungana na magwiji hao baada ya yeye jana usiku kufanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa barani ulaya ambayo ilipigwa nchini Uingereza kwenye jiji la London, Ambapo ni ardhi ya nyumbani ya kiungo huyo fundi.

bellinghamKiungo huyo amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Real Madrid baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Spanish Super Cup, La Liga, pamoja na ligi ya mabingwa narani ulaya ambapo ni msimu wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo bora kabisa duniani.

Acha ujumbe