Modric, Carvajal, na Nacho Waandika Historia Madrid

Wachezaji watatu wa klabu ya Real Madrid Luca Modric, Nacho Fernandez na Dani Carvajal wameandika historia ndani ya klabu hiyo baada ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya sita wakiwa ndani ya klabu hiyo.

Luca Modric na wenzake hao wawili wanaingia kwenye historia ya klabu hiyo kama wachezaji pekee waliotwaa mataji sita ya ligi ya mabingwa ulaya tangu michuano hiyo ifanyiwe marekebisho mwaka 1992.MODRICWachezaji hao wamekua kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kimetwaa mataji sita ya ligi ya mabingwa ulaya kwa miaka (10) iliyopita ambapo ni mwaka 2014, 2016,2017,2018,2022, na mwaka 2024 ikiwa hakuna wachezaji wengine waliowahi kufanya hivo.

Ikumbukwe pia mchezaji Toni Kroos ambaye amecheza mchezo wake wa mwisho kwenye fainali ya jana nae ametwaa mataji sita ya ligi ya mabingwa barani ulaya, Lakini yeye akiwa ametwaa mataji matano tu ndani ya klabu ya Real Madrid, Huku taji moja akitwaa na wababe wa soka la Ujerumani klabu ya Bayern Munich.MODRICKiungo Luca Modric na beki Nacho Fernandez licha kua wachezaji pekee kushinda mataji sita ya ligi ya mabingwa ndani ya Real Madrid, Lakini pia wameandika rekodi nyingine baada ya kushinda taji la ulaya usiku wa jana na kua wachezaji walioshinda mataji mengi zaidi klabuni hapo wakifikisha mataji (26) wakimpita beki Marcelo mwenye mataji (25).

Acha ujumbe